Utamtambua mwanamke kwa maumbile yake, na ndivyo pia kwa mwanamume. Mwanamke anapozungumza, basi utamfahamu hata kabla ya kumuona, na ndivyo pia na mwanamume.
Lakini, kutana na Kezia Njeri mwenye umri wa miaka 53, maumbile yake hasaa sura, na kuongea utasema ni mwanamume, lakini ni mwanamke na mama ya mtu . Hata hivyo, amekuwa na wakati mgumu kuwaambia walimwengu yeye ni mwanamke, kwani wengi hawaamini. Siku moja ilibidi maafisa wa polisi wamvue nguo waamini ni mwanamke baada ya kumkamata .
No comments