Watu nchini Marekani wameelezea ghadhabu na hasira zao kwenye mitandao ya kijamii kufuatia utafiti wa mtaalamu wa wanyamapori Paul Roslie kumezwa na Nyoka aina ya Anaconda ili ku chunguza maumbile ya ndani ya Nyoka huyo.
Lengo la utafiti huo ambao ulikuwa wa kwanza wa aina yake duniani, ilikuwa ni kuchunguza maumbulie ya ndani ya Nyoka huyo anayepatikana katika msitu wa Amazon.
Hata hivyo inaarifiwa bwana Paul alilazimika kusitisha utafiti wake ambao umezua utata muda mfupi tu baada ya kuuanzisha.
Watu nchini Marekani walijionea kwenye televisheni zao kipindi kilichokuwa kinapeperushwa cha mtaalamu huyo kuingia ndani ya tumbo la Anaconda akiwa amevalia vazi maalum ambalo yangesaidia kuchunguza kiwango cha joto mwilini mwake na pia kupima mipigo ya Moyo wake wakati akiwa ndani ya tumbo la Nyoka huyo.
Paul na vazi alilotumia kuingia ndani ya Nyoka kabla ya kushindwa na kusalimu amri
Rosolie na kikundi cha wasaidizi wake walipata Nyoka ya Anaconda mwenye uzito wa kilo 180, walipokuwa katika msitu huo. Alipanga kuwa ataonyeshwa kwenye stesheni hio akiwa anamezwa mzima mzima na Nyoka huyo.
Rosolie alionekana akiingia ndani ya mdomo wa Anaconda kwa kichwa chake huku wenzake wakimtazama.
Alikuwa amevalia vazi maalum lenye Carbon na likiwa limepakwa damu ya Nguruwe, kabla ya kujielkeza kwa Nyoka huyo kama mlo wake.
"sikutana kumhangaisha mno mnyama na pia mimi mwenyewe sikutaka kujiumiza. ''
Paul anapenda sana kujihusisha na maswala ya wanyama hasa Nyoka
"nilitaka kuhakikisha kuwa vazi langu halitamjeruhi Nyoka huyo kwa vyovyote vile.''
''Mimi mwenyewe sikuogopa hata kidogo. Watalaamu walifanyia jaribio vazi langu, kwa hivyo tulijua kuwa halitamwathiri kwa vyovyote Nyoka huyo. ''
Lakini baada tu ya saa moja ya mtaalamu kuingia ndani ya tumbo la Nyoka na kuanza kubanwa, aliamua kusitisha utafiti wake akihofia kuwa angeumizwa na Nyoka huyo mkubwa. Alisikika akiwaita wenzake kwa kifaa maalum cha kupaza sauti kilichokuwa kimewekwa kwenye vazi lake na kuwamabia kuwa anaumizwa.
''Nahisi kama mifupa yangu inasagwa sagwa, njooni mniondoe hapa.'' alisema Paul.
Namna ambavyo Rosolie aliponea kufa baada ya kubanwa na Nyoka huyo bado ni muujiza ingawa aliweza kupata hewa kutokaa kwa vazi lake hilo kwa saa tatu.
No comments